Viva Forums
Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.
Viva Forums

Welcome to Viva Forums


You are not connected. Please login or register

Mhubiri apata almasi ya mamilioni ya dola

Go down  Message [Page 1 of 1]

magison



Mhubiri mmoja wa kikiristo amepata moja ya almasi kubwa zaidi kuwa kupatikana duniani kwenye wilaya ya Kano nchini Sierra Leone.

Almasi hiyo yenye uzito wa karati 709 kwa sasa imefungiwa kwenye benki kuu nchini Sierra Leone mjini Free Town. Ni moja ya almasi 20 kubwa zaidi kuwai kupatikana.

Wachimba migodi wa kujitegemea ni wengi kwenye migodi yenye almasi nyingi nchini Sierra Leone.

Lakini kuna maswali ikiwa jamii itanufaika kutokana na kupatikana kwa almasi hiyo.

Almasi hiyo iliyogunduliwa na Emmanuel Momoh ambayo thamani yake bado haijatangazwa ndiyo ya pili kubwa zaidi kuwai kupatikana nchini Sierra Leone tangu mwaka 1972 wakati almasi nyingi ya karati 969 ilipatikana. Kwanza ilipelekwa kwa Rais Ernest Bai Koroma siku ya Jumatano kabla ya kupelekwa benki kuu.

Rais alimshukuru Chifu wa eneo hilo na watu wake kwa kutoisafirisha almasi hiyo nje ya nchi.

Bwana Koroma alisema kuwa wamiliki wa almasi hiyo watapata haki yao na itainufaisha nchi.

Sierra Leone ni maarufu kwa sekta ya almasi.

Biashara ya almasi ilichochoea vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muongo mmoja wakati makundi ya waasi yalifanya biashara ya kubadilishana almasi na silaha

Chanzo: BBC Swahili

Back to top  Message [Page 1 of 1]

Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum